Lynn Akiri Kuwahi Kuwa na Tabia Ya Udokozi
Video vixen maarufu ambaye sasa ni Msanii wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis maarufu kama Lynn amefunguka na kuweka wazi kuwa aliwahi kuwa na tabia ya udokozi.
Mrembo huyo ambaye amewahi kuwa Mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, ametoa siri jinsi alivyokuwa anapenda kula maziwa ya unga kiasi kwamba alikuwa anadiriki kudokoa pesa za mama yake ili mradi tu akanunue maziwa hayo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Lynn alisema alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kulamba maziwa ya unga, ikawa asipoyapata anakosa amani hivyo alifanya kila awezalo apate pesa akayanunue.
“Yaani nilikuwa napenda sana kulamba maziwa ya unga kiasi kwamba nilianza kuwa na katabia ka’ kudokoa pesa za mama ilimradi tu nipate maziwa ila ikafika wakati mama ikambidi azoee hiyo hali, akawa ananipa pesa nikanunue ili nisizoee tabia ya wizi”.
Lynn Alipay’s umaarufu Baada ya kuwa video queen kwenye wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ na Hivi karibuni ametoa wimbo wa kwanza na kutangaza rasmi kuingia kwenye muziki.