Lynn Afungukia Mapenzi Yake Kwa Jacqueline Wolper
Video Vixen na msanii wa Bongo fleva Irene Louis maarufu kama Lynn amefunguka na kuweka wazi kuwa anamkubali sana mwanadada mkali wa fasheni Jacqueline Wolper.
Lynn alifunguka hayo Baada ya kuulizwa sababu iliyomfanya Mpaka awe namfuatilia Msanii mmoja tu Bongo kupitia ukurasa wake wa Instagram na sio wasanii wengine.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari nchini, Lynn ameweka wazi kuwa sababu ya kwanza ni kuwa anamkubali sana Wolper na pili ndio mtu ambaye kibongo bongo anaendana naye:
Mimi naona toka tujuane tunakuwa tupo sawa tu kishikaji tunaongea, kwa hiyo yeye kama kuna kitu tumefanana ndio maana tumekuwa hivyo. Nahisi damu zetu zimeendana, labda wengine watakuja”.
Siku chache zilizopita Jacqueline Wolper alifabya bonge la party kwa ajili ya kusherehekea miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake, Mwanadada huyo ( Lynn) ni miongoni watu waliojumuika.