Lyn Anyoosha Mikono kwa Tanasha
Mwanadada Irene ambae alikuwa video vixen na kwa sasa amejiingiza katika anga za muziki amefunguka na kusema kuwa kwake haoni tatizo kama Diamond ataamua kumuoa mwanamke aliyenae sasa katika mahusiano kama ambayo mwanaume huyo ametangaza ndoa hivi karibuni.
ikumbukwe kuwa irene aliwahi kuwa katika mahusiano na Diamond platinumz , lakini kwa sasa mwanadada huyo haijulikana yukpo na nani huku akimuacha Diamond akipeperuka kwenda kwa mwana dada kutoka nchini Kenya,
sina kinyongo, Diamond amuoe Tanasha hata kesho maana ni jambo la kheri kabisa, nitafurahi sana kwa sababu diamond ni mshikaji wangu sana na sio vinginevyo.
Mara zote mwanadada huyo hajawahi kukubali kuwa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na Diamond platinumz, zaidi ya kusema kuwa ni marafiki na watu wa karibu tu.