Lulu Diva Awachana Walikuwa Wakimwita Gumegume
Mwanadada Lulu Abas maarufu kama Lulu Diva anaefanya vizuri katika anga za muziki wa bongo fleva amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwashangaa sana baadhi ya watu waliokuwa wakimwita gumegume kipindi cha nyuma na kwamba ni muhuni hawezi kutulia na mpenzi mmoja kitu ambacho yeye anasema kuwa wala haijawahi kuwa tabia yake.
Lulu Diva amesema kuwa kipindi anaanza mahusiano na mpenzi wake aliyenae sasa hivi , huku akikataa kutaja jina la bwana huyo watu wengi wakimkuwa wakimwita gumegume hasa marafiki zake na kumwambia kuwa hawezi kudumu nae kwa muda mrefu kwa sababu yeye ni gumegume hajazoea kukaa na bwana mmoja muda mrefu.
Akiongea na ijumaa wikienda Lulu Diva anasema kuwa watu hao kwa sasa akiwaangalia na akinagalia mahusiano yake yalivyofika mbali tangu walipokuwa wanaanza kuongea anawacheka tu kwa dharau
kuna watu walikuwa wakiniita mimi gumegume na kwamba eti siwezi kukaa na mpenzi mmoja na nikadumu nae,kama nilivodumu na huyu mpenzi wangu wa sasa hivi.Ninawangaliaga alafu nawacheka kwa dharau-Alifunguka mwandada huyo machachari katika kazi yake.
Ingawa ni kweli kwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakishndwa kukaa na mpenzi mmoja kwa muda mrefu na hii inawezekana ikawa ni moja ya sababu ya marafiki zake kuwa wakimwita gumegume, hapo awali Lulu Diva alikuwa akitoka kimapenzi na msanii mwenzie Ney wa mitego ambapo walikuja kuachana na kuwa watu wa karibu tu.
wasanii wengi wamekuwa wakishindwa kudumu katika mahusiano ya mapenzi ma wenzi wao na kuwa wakiruka ruka kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine huku mbaya zaidi wakiwa wanatembea wasanii wenyewe kwa wenyewe na hii ndio maana inakuwa kazi kuwa na mahusiano ya kudumu ndani ya bongo hasa kwa wasanii wa muziki.