Lulu Diva Arudisha Pesa ya Mahali Kwa Mume.
Msanii wa kike wa muziki nchini Lulu Diva amerudisha pesa aliyotolewa ya mahali kutoka kwa mpenzi wake ambae alipanga kufunga nae ndoa.Lulu Diva amerudisha pesa hiyo kwa mwanaume huyo aliedumu nae kwa muda wa miaka mitatu.
Kwa habari zilizokuwa chini ya kapeti zinasema kuwa Lulu Diva alitakiwa kufunga ndoa tangu mwaka jana mwishoni lakini mwanaume huyo aliona kuwa haitawezekana baada ya kusikia tetesi kuwa mwanadada huyo anatoka kimapenzi na msanii mwenzie Rich Mavoko.
kama kuolewa basi mwanadada huyo alitakiwa kuolewa mwaka jana mwishoni lakini mwanaume huyo alibaini kuwa anatoka kimapenzi na msanii mwenzie rich mavoko, kwaio akaomba kurudishiwa mahali yake.
Hata hivo Lulu Diva alipigiwa simu na kuulizwa kuhusu swala hilo na alijibu kuwa ni kweli kuwa alirudisha mahali ya mwanaume aliyetaka kumuoa lakini sio kweli kuwa aligundua kuwa ana mwanaume mwingine bali alipata shinikizo kutoka kwao kuwa yeye sio mwanamke wa kuoa.
Aliposhinikizwa sana nikaona isiwe tabu,nikamrudishia mahali yake maana alikuwa akiwasikilza sana ndugu zake ambao walikuwa hawataki anioe.
Hivi karibuni Lulu Diva na Rich Mavoko wamekuwa wakionekana kuwa karibu sana na hata kuhisiwa kuwa waili hao watakuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Picha ya hivi karibuni ya Rich Mavoko na Lulu Diva