Lulu Diva Amefunguka Kuhusiana Bwana Anayemgombania na Gigy Money
Msanii kike wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa, Lulu diva ameongelea bifu au ugomvi unaosemekana upo baina yake na msanii mwenzake anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Papa’ Gigy Money huku ikidaiwa Kisa kikubwa cha bifu hilo kikiwa ni mwanaume.
Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva na Gigy Money hawapikiki chungu kimoja hata kwa sekunde moja na hata wakikutana sehemu hawawezi kuzungumza lakini pia inadaiwa Kisa na mkasa ya uhasama huo ni kuwa kuna mwanaume ambaye warembo hao wote wawili wanamtaka kwa wakati mmoja kitu kinacho sababisha mikwaruzano.
Tetesi hizi zilizidi hasa hapa Kati baada ya warembo hao kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii, kwenye mahojiano na East Africa Tv kupitua kipindi cha Enews, Lulu Diva alikana kata kata taarifa hizo na kudai kuwa hana ugomvi na Gigy Money:
Amchukue bwana angu ampeleke wapi labda? Kwanza mi nawashangaa sana mimi sinaga ugomvi na Gigy Money na wala sijawahi kugombania naye bwana labda saa nyingine maneno yanavyo ongelewa inakuwa ni showbiz tu lakini mimi na Gigy Money tunajuana wenyewe ananipenda na mimi ninampenda yaani in short tunapendana na pia tunasapotiana kwenye kazi zetu mimi naimba nyimbo zake na vice versa yaani tupo fresh kabisa halafu isitoshe mwanaume wangu hana time na wait walio kwenye media mimi mwenyewe nimejuana naye kabla sijawa staa yaani Nina uhakika ningekutana naye wakati nimekuwa maarufu asingenitamani”.