Lulu Diva Akanusha Kuishi Kwa Kudanga.
Msanii wa kike wa miondoko ya mduara Lulu Diva hivi karibuni amekuwa akikumbwa na tetesi nyingi za kutupa mtoto mara za kuishi mjini kwa kutegemea wanaume na vitu vingine vingi.hata hivyo msanii huyo amefunguka na kusema kuwa sio kweli kuwa amekuwa akiishi kwa kudanga kwa sababu maisha mazuri kwake yamekuwepo kwa muda mrefu.
Kwanza kabisa mimi maisha ninayoishi ni mmazuri kabla hata sijawa hata mwanamuziki, nilikuwa hivi hivi tangu zamani.mimi ni msichana niliyehangaika sana kutafuta maisha , nilishawahi kuwa waiter, nikafanya baaadhi ya biasghara.nimeshahangaikia sana pesa yangu na wala sijawahi kudanga, tangu zamani nilikuwa nahangaikia sana maisha yangu tangu zamani.
Lulu Diva pia amekanusha stori kuwa amechukuliwa na pedeshee ambalo limemuweka mjini na kumpa kila kitu