Lulu Diva Ajitabira Ndoa na Mtoto 2019
Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye mwaka huu alifanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Diva amefunguka na kusema mwakani ana ndoto ya kuzaa na kuolewa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Lulu Diva amefunguka kuwa kwa kazi yake ya muziki anayoifanya hivi sasa, kufanya kitu ambacho huko mbeleni hakitampa kikwazo kama kupata mtoto mapema ili akiwa anaendelea kumtafutia maisha, yeye anaendelea kukua.
Ni vizuri sana kujipangia malengo ya kimaisha na mimi ndiyo hivyo nimeshapanga ninachokitaka mwakani kwa sababu maisha yenyewe ni mafupi. 2019 nikifanikiwa kupata ndoa ni heri, lakini hata kama nitapata mtoto nitashukuru pia”.
Mwaka huu ulianza kwa tetesi za Lulu Diva kuolewa lakini taarifa hizo ziliyeyuka Baada ya Lulu Diva kuachwa na mchumba Wake Baada ya kuenea kwa tetesi za mahusiano na Rich Mavoko.