Lulu Diva Afungukia Tetesi Za Kufilisika
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka amefunguka kuwa watu wanaomsema amefulia watakuwa hawamuelewi vizuri.
Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva amefulia kupita kiasi kutokana na kutosikika kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alisema watu wanaodhani mtu akiwa anajinadi kwenye mitandao ya kijamii, basi ndiyo maisha yake ya kweli anayoishi, wanajidanganya hivyo kwa sababu hawaoni nikifanya hivyo kama mwanzoni ndiyo wanaona kafulia.
Unajua watu wanapenda sana kudanganywa mitandaoni ndiyo maana macho yao yanaangalia wale wanaojionesha na vitu feki, lakini kama mtu ametulia watasema amefulia, hapo nashindwaga kuelewa kabisa, niwaambie tu sijafulia na siwezi kwa sababu ninajitambua”.