Lulu Adaiwa Kuwekewa Bodyguard Baada Ya Kuvishwa Pete
Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amedaiwa kuwekewa ulinzi mzito na mume wake mtarajiwa Majizzo Baada ya kumvalisha pete.
Gazeti pendwa la Amani linaripoti kuwa tangu Lulu avalishwe pete ya uchumba na kuwa mke mtarajiwa, aliwekewa ulinzi huo binafsi hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.
Nafikiri jamaa wake kaona ni vizuri kwa vile Lulu ni staa na kumtengenezea muonekano wa kistaa, ni vizuri akawa na mlinzi binafsi, sasa hivi ana bodigadi anaitwa Livingstone“.
Gazeti hilo lilithibitisha taarifa hizo wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho kwenye jengo la LAPF baada ya kumnasa msanii huyo akiwa na bodigadi huyo mwenye ‘miraba minne’ alipokuwa amehudhuria kwenye harusi ya jamaa anayefahamika kwa jina la Renatus Nyakai na mkewe Glorian Jarimo.
Mmoja wa shabiki wa Lulu aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Mnyate aliyeshuhudia jinsi Lulu alivyokuwa akilindwa, alipongeza na kusema anastahili kwani ni staa mkubwa.
Unajuwa Lulu ni kipenzi cha watu sana na zamani hatukuwa tumezoea hivyo ilikuwa kila akionekana watu tunajifotolesha mapicha lakini kwa sasa haya nafikiri ni mabadiliko mazuri kwani ni staa mkubwa“.
Tangu ametoka gerezani miezi Michache iliyopita Lulu amekuwa na upepo wa bahati nzuri kwani amechumbiwa na Mpenzi Wake wa muda mrefu Majizzo na kumaliza kifungo chake rasmi.