Lucy Komba awapasha mashabiki wa Zari wanaomtusi Hamisa Mobetto
Muigizaji wa bongo Lucy Komba amefunguka kwa mara ya kwanza kuwakomesha watanzania ambao wanamtukana Hamisa Mobetto kisa kuwa mtoto aliyezaa ni Diamond Platnumz.
Hii ni baada ya wengi kudai kuwa kunauwezekano wa mtoto huyu wa pili wa Mobetto kuwa wa Diamond Platnumz ambaye anasemekana aliwahi kutoka kimapenzi na Hamisa Mobetto.
Hata hivyo Lucy Komba aliwatoa wengi povu kwa kuandika;
“Samahani lakini kimenichoma. MABOGAS YA TZ YANAMPONDA MTZ MWENZIO YANAMSIFIA BOGAS MWENZIO sijui yanafikiri yatapewa ule urithi. Mbona waganda hawambabaikii acheni umasikini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga moja moja ya bure,”
Aliongeza,
“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu. Wale wanaoniponda eti ningekuwa mzalendo nisingeolewa na mzungu, Yes nimeolewa na mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wakisfrika kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B. Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataharifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia insta na kuzizungusha bado hajawapata taarifa za kunichamba huku mmesimaisha visimi. Ukweli unauma mmepewa ukweli wa huyo stranger wenu aliyenenepesha miguu kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia chambeni tu mniongezee followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa bongo unatokana na vichambo. GOODMORNING.,”