Linah:Huwezi Kubadili Dini Kwa Sababu Ya Mapenzi

Mwanadada aliyekuwa anafanya vizuri katika muziki wa kizazi kwa mud mrefu nyuma ambae kipaji chake kilitengenezw a vizuri kutoka THT , jumba kubwa lenye vipaji Linah Sanga amefunguka kuwa ni vigumu kwa mtu kubadili dini kwa sababu ya mapenzi na inawezekana ni kweli kuwa dini  imekuwa ni kikwazo kwa watu wengi kushindwa kufanikisha ndoto hiyo.

Hata hivyo mwanadada huyo ambae yuko kwenye mahusiano na mwanaume ambae wanatofautiana dini huku Linah mwenyewe akijulikana kuwa ametoka katika familia ambayo wanaamini sana dini kwa upande wa kikristo alishawahi kusema kuwa hata kama  mwanaume huyo aliebahatika nae kupata mtoto mmoja wana dini tofauti haimaanishi kuwa watashindwa kuishi pamoja.

download latest music    

Mwanadada huyo anasema kuwa swala la kubadili dini iwe ni sababu ya imani yako kukutuma kufanya hivyo lakini sio kubadilisha dini kwa sababu ya kufata mapenzi kwa mtu fulani.

Unajua kiimani utakiwi kufanya vitu juu juu,na hata kama unataka kubadilisha dini basi iwe ni kwa sababu ya dini na imani yako lakini sio kwa sababu ya mapenzi hata siku moja, kwaiyo mimi sikutaka kufanya iyo michezo ila ninaamini kuwa  patalegea tu popote pale au tutfunga ndoa hivyohivyo na Mungu mwenyewe atalegeza kwa sababu tunapendana na tayari tuna mtoto anaetuunganisha kwa hilo.-Alifunguka Linah

Hata hivyo katika kuongezea swala hilo Linah alisema kuwa kwa upande wa familia ,familia zote zimekuwa ni ngumu kukubaliana kwa sababu pande zote zimejidhatiti katika dini yao,

Kwetu nahisi ndio sana japo kwao kwao pia ni wagumu lakini nahisi ni kotte kote tu maana kwao ni waislamu sana na sisi ni wakristo sana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.