Linah Sanga Azidi Kukwepa Tetesi Za Kumwagwa na Baba Watoto Wake
Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Linah Sanga amezidi kukwepa tetesi za kuwa ameachana na Mpenzi na mwanaume aliyezaa naye Mtoto Wake wa kwanza Shaban Mchomvu.
Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa Linah na baba watoto wake wameachana Baada ya Shabani kuchoshwa na maisha ya kimuziki anayoishi Linah ikiwemo mavazi ya ajabu.
Lakini Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi Enews cha EATV, Baada ya kuulizwa kuhusu taarifa hizo Linah amekuja juu na kuwataka watu wafatilie muziki Wake na sio maisha yake binafsi.
Sidhani kama mashabiki zangu wanatakiwa kufahamu kuhusu maisha yangu binafsi, wanachopaswa kukifahamu ni muziki wangu tu kwaiyo siwezi kuzungumzia hilo”.
Linah ametangaza kutoa wimbo wake mpya hivi karibuni na kuwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani video ya wimbo huo imeshakwisha kamilika.