Linah Sanga Ataja Hadharani na Bwana Mpya
Msaniibwa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga anadaiwa kutoka hadharani na Mpenzi mpya marabaada ya kuachana na baba watoto wake Shaban Mchomvu.
Gazeti la Ijumaa Wikienda wanaripoti kuwa Linah alijiachia na jamaa huyo mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Iringa alipokuwa anashiriki kwenye tamasha la Wasafi Festival.
Linah aliachana na baba mtoto wake miezi kadhaa iliyopita alionekana kwa mara ya kwanza na mwanaume mwingine ambapo mashuhuda waliwashuhudia wakiwa wamegandana kama ruba kwenye kila kona mjini Iringa.
Baada ya Linah na kijana huyo kuonekana wakiwa na ukaribu usio wa kawaida Gazeti la Ijumaa lilimfuata na kumhoji kuhusu uhusiano wao ambapo mara moja alimwaga Povu zito:
Sitaki mambo ya umbeya, kwa hiyo nisiambatane au kukaa na mtu? Kwanza sioni cha ajabu kwa sababu sasa hivi nipo huru na mambo yangu, naweza kufanya chochote ninachojisikia na hakuna wa kuniwekea mipaka katika uhusiano wala kazi zangu, niacheni na mambo yangu tafadhali”.
Linah aliachana na mzazi mwenzake Shabani Mchomvu Baada ya kuzaa naye Mtoto mmoja mwenye mwaka mmoja anayeitwa Tracy Paris huku sababu za kuvunjika kwa Penzi Lao zikiwa hazijawekwa wazi.