Linah na Amini Wadaiwa Kulifufua Penzi Lao
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Linah sanga na msanii mwenzake kutoka THT Amini wamedaiwa kurudisha Penzi Lao kama zamani Baada ya kuwa wameachana kwa muda mrefu.
Amini na Linah wamerudi kwenye headlines na sasa kuna tetesi kuwa wamerudiana huku tetesi hizo ziiibuka Baada ya Linah kuonekana kuwa karibu na muimbaji huyo wa wimbo, ‘Nisahaulishe’ na anaenda mbali zaidi kwa kujirekodi vipande vya video vinavyohashilia ni meseji za mahaba mazito.
Lonah ambaye ni mama wa Mtoto mmoja aliyezaa na aliyekuwa Mpenzi Wake Shabani Mchomvu ambaye amekiri kuwa wameachana kwa miezi karibuni Tisa na kudai yuko single.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Bongo 5, Amini alifunguka na kuzungumzia tetesi hizo za kurudiana na aliyekuwa Mpenzi Wake ambapo alisema:
Mapenzi ni kikohozi kama ni kweli mtaona kila kitu”.