“Labda nina mimba ya Wizkid” Gigy Money asema
Msanii na mrembo wa video Gigy Money amekuwa akisingiziwa kuwa anamimba kitu ambacho aliweza kufunguka kuhusu hivi karibuni.
Akizungumza na FNL ya EATV Gigy Money aligusia kuhusu wimbo wake mpya ‘Papa’, alafu baadae akaongeza kwa kana taarifa zinazodai kuwa anamimba huku akisema kuwa ameiambia FNL ya EATV kuwa anatamani sana kutoka kimapenzi na msanii Wizkid ambaye anaweza kumzalia.
“Kipindi cha sasa hivi na Papa ndio nimetoa?, hapana, ujue mpaka yananishtua maneno haya, you know sina mimba lakini labda nina mimba ya Wizkid unajua mimi natamani ikaenda ikashuka tu.”
Akamalizia kwa kusema;
“Yeah namkubali, unajua dream sio wote wanatimiza ndoto zao, mimi nimetimiza ndoto yangu, nilisema Tekno moyoni siumeona huyu hapa akajaa,”