“Kwa sasa kunilinganisha na akina Amber Lulu na Gigy Money ni dharau kubwa, si levo zangu, tazama muziki wanaofanya na muziki wangu” Lulu Diva
Lulu Diva amepanda cheo na sasa hataki kuwa analinganishwa na video vixen wengine kama Amber Lulu and Gigy Money.
Mwanadada huyo aliyekuwa video vixen hapo awali sasa hataki kamwe kuekwa kwenye levo moja na watu wengi kwa sababu anafanya mambo makubwa.
Akichonga na Mikito Nusunusu, Lulu alisema ni kweli wapinzani wake wote hao wanafanya muziki kwa sasa kama anavyofanya yeye lakini bado levo zao si kama zake maana yeye yupo chini ya uongozi unaosimamia kazi zake za kimuziki na umemuwezesha kupata kolabo nje ya nchi na Mzimbabwe Jah PPrayzah.
“Kwa sasa kunilinganisha na akina Amber Lulu na Gigy Money ni dharau kubwa, si levo zangu, tazama muziki wanaofanya na muziki wangu” alimalizia.