Kwa Roma Naomba Wamfikirie Mara Mbili: Nay wa Mitego.
Msanii Ney wa Mitego amefunguka kuhusu kupewa onyo baada ya nyimbo zake kufungiwa katika vyombo vya habari.Ney wa Mitego ni msanii anaeongoza kuwa na nyimbo nyingi katika orodha ya nyimbo zilizotolewa na Baraza la Sanaa.
Akizungumza na Cloud e, Ney wa Mitego anasema kuwa kwa upande wake anaona kabisa kuwa nyimbo yake mpya ya mikono juu haikustahili kuwepo katika orodha hiyo kwa sababu ukisikiliza ngoma hiyo iko tofauti na nyimbo zake za nyuma ambazo amekuwa akiimba.
wimbo wangu mmoja upo pale kimakosa, haukutakiwa kufungiwa kabisa ukimsikiliza ney huyu wa mikono juu sio yule wa zamani, audio ya makuzi tulishairekebisha , nilikaa na baraza na tukaongeana na tulishamaliza.
Nay wa mitegoanasema kuwa amekuwa akitumia tasfida katika muziki wake kila mara lakini kitu kinachomkosesha amani ni kwamba watu wanafumbua tasfida na yanakuwa maneno ya kawaida.
natumia tasfida sana,kama unafumbua tasfida hilo ni tatizo lako na kama nispotumia tasfida nitatumia nini sasa.
Hata hivyo Nay wa Mitego anasem akuwa wimbo wa mikono juu ni wimbo mpya ambao ndo kwanza unaanza kupokelewa,baraza limeshindwa kutambua na kuniambia tatizo la wimbo wangu labda tukikutana tena wiki ijayo.
Tumezungumza kuhusu mabadiliko na mpaka nimetaka kujua tatizo la mikono juu na tumekubaliana nibadilishe.nina imani hauna tatizo na wao hawajasema tatioz liko wapi ila kila list imeshazoeleka kwa ni lazima ney wa mitego atakuwepo.tumeyamaliza na tumekubaliana kufanya muziki mzuri na kufanya mabadiliko katika muziki.
Nay wa Mitego pia alipata nafasi ya kuzungumzia swala la Roma ambae yeye pia amefungiwa muziki wake na pia hapaswi kufanya kazi kwa muda wa miezi sita.
tunaishi kupitia muziki, pengine labda tungekuwa vibaka, wezi, au jela au hata tushakufa.mtu anakosea lakini kwa sababu tuna wazazi inabidi wawepo kuturekebisha lakini kwa kutuambia pale tunapokosea na mtu ajiridhishe na kosa lenyewe kwanza.Nimewahi kufungiwa najua maumivu yake, sitaki kuliongelea sana hili lakini kwa Roma naomba wamfikirie mara mbili.