Kundi la Makomando Lasambaratika,Kila Mmoja Aamua Kujitegemea.
Makomandoo ni moja ya makundi makubwa ambayo yalikuwa yanategemewa kufika mbali lakini sio kilakinachotegemewa kinaweza kwenda kama kinavotakiwa kuwa, ndivyo ilivyo kwa kundi la makomando ambalo sasa hivi itaaanza kusikika kila mmoja akifanya kazi peke yake na chini ya uongozi wake.
Akithibitisha hilo moja ya wasanii wa kundi hilo Fredy Whine amesema kuwa kwa sasa mwenzake Muki yuko busy nyumbani na mambo yake hivyo kwa upande wake hawezi kusubiria mpaka Muki akitaka kufanya kazi tena.Hata hivyo Fredy Whine nae kwa sasa yuko chini ya menejiment mpya inayomsimamia kazi zake.
Yeye yuko kwake anafanya kazi zake, siwezi kusubiria amalize mambo yake tufanye wote, na mimi am musician kwaio acha nifanye .tulikutana tukashare ideas kwaio nitafanya.so its not makomando, its me new boy ,unapona mtu yko busy na mambo yake inabidi ufanye yako.Yeye kwa sasa ana familia yake, na mimi nilikuwa nayo na ninayo lakini ya kwake ni ngumu zaidi.
Kuna project nyingi nilikuwa nafanya mwenyewe , kuna wimbo nimeimba nikautoa nikauleta makomandoo sauti yake haipo lakini hakuna aliyejua,Wengi walikuwa wakisema kuwa alikuwa ananibeba lakini sasa hivi ni muda wangu kuwaonyesha kuwa mimi pia ninaweza kuliko.
Nae meneja mpya wa Fredy, Henry Ado Mapunda anasema kuwa makomandoo ni moja ya kundi alilokuwa akilipenda sana na amesikitika sana kuiskia kuwa wanshindwa kuendelea kuwa wote tena lakini pia anaona bora kumchukua fredy na kufanya nae kazi kwa sasa.
Nilikuwa nawapenda sana makomandoo, nimesikitika sana sana kama wamevunjika na hata aliposema kuwa yuko free nikaona let come together na tufanye kitu pamoja.tuko na ziggy zaggy from Nigeria watafanya kazi kwa pamoja na wiki ijayo Fredy Whine atafanya events Kigali.
Makomandoo walianza muziki wakiwa kundi la watu wanne baadae wawili walikuja kuondoka na kubaki wawili ambao wamekaa zaidi ya miaka 10 pamoja na sasa hivi familia imewatenganisha, wameshindwa kufanya kazi pamoja kwa sababu Muki sasa hivi ana kabiliwa na maswala ya kifamilia.