“Kuna kipindi nilikosa hata nguo za kuvaa” Rayvanny asimulia safari yake kimuziki baada ya kushinda tuzo la BET

Rayvanny alifunguka kuhusu maisha yake ya awali kabla ya yeye kuwa mtu mashuhuri na kupata hela. Staa huyo wa Wasafi aliamua kuongea kuhusu maisha yake ya awali baada ya kushinda tuzo la BET.

Ray alimshukuru sana Madee ambaye alisema alimsaidia sana wakati bado alikua fukara, staa huyo aliishi na Madee alipokuja Dar kutafuta riziki.

download latest music    

“Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi Ambacho nilikutana na Unaemuona mbele yangu.kipindi hicho Sikujua nilichonacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye.Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam.Lakini kaka angu @madeeali Alisimama namimi Kila Alipokua Akienda Alienda na mimi na hii yote ni baada yakuniona mnyonge Nisie na msaada.Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu @madeeali Pia Alikua akinipeleka studio nakunishauri Vitu vingi sana vyakimaisha na mziki pia nakusisitiza kua Nisikate tamaa.

Rayvanny na Madee

 

“Nimepata Uzoefu Mkubwa wakutumbuiza mbele ya kundi la watu kutoka kwake.Kuna kipindi nilikosa hata Nguo zakuvaa Alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.Nakumbuka kuna kipindi Akasema mdogo wangu Ray jifunze gari,nikamkatalia nakumwambia kwamba mimi ntaendesha Wapi gari na Ntakuja lini kupata gari.Akaniambia mdogo wangu Unakitu Ambacho kitakusaidia baadae yote yatawezekana.Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini Alinivumilia hadi nikajua Pia Nikawa mjanja wavitu vingi na kujiamini kisa yeye.Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio Alikua mstari Wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae Akichangia mpaka #Raymondtiptop Akawa #Rayvanny Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani #BETAwards MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA…. HUU MWANZO MUNGU MWEMA @madeeali” Rayvanny aliandika.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere