Kuhusu Picha Za Utata Na Mobeto,Petitman Afafanua
Ikiwa ni kama wiki sasa imepita tangu sakata la Hamisa mobeto Diamond kunyamaza na kutulia , kumeibuka kwa picha zingine katika mitandao huku zikimuonyesha tena Hamisa na mwanaume mwingine katika hali ya mahaba. Kabla ya kuvuja kwa picha hizi mpya, mara ya kwanza zilisambaa baadhi ya picha zikimuonyesha Hamisa akiwa na msanii Diamond katika hali ya mahaba ikiwa kama ushahidi wa kuwa wawili hao walikuwa wapenzi huku pia ikiwa ni kama njia ya Hamisa kujitetea kwa jamii baada ya Diamond kumkata mtoto aliyejifungua hivi karibuni, picha hizo zilitoa msukumo mkubwa kwa Diamond kukiri kuwa ni kweli alikuwa na mahusiano na mwanadada huyo na kukubali majukumu ya mtoto.
Juzi tena zimeibuka picha mpya, zikimuhusisha mwanadada yuleyule Hamisa mobeto akiwa na mtu mwingine maarufu katika tasnia ya Bongo Fleva lakini akiwa pia mtu wa karibu na familia ya Diamond , Petitman , ambae ni meneja wa msanii anaefanya vizuri sasa katika muziki Country boy, pia ni mtu wa karibu na msanii wa Bongo Movie Madam Wema Sepetu pia ni mume wa dada yake msanii Diamond anaejulikana kama Esma Platinumz.
Petitman alipoona kumekuwa na maneno mengi yakiongelewa kuhusu picha hiyo bila kuwana ufafanuzi kutoka kwa mtu yeyote, aliamua kufunguka na kusema yanayohusu picha hiyo,”picha zinazosambaa kwenye mitanda ya kijamii ni za zamani sana.hazina uhusiano wowote na maisha yangu yangu ya sasa au yale yanayoendelea kuhusu Hamisa ambae pia anaonekana katika picha hizo kwa sasa.yoyote ambae ameamua kuzisambaza ana nia moja tu kuniunganisha katika swala ambalo sihusiki na kunichafua.mimi kwa muda mrefu niko na mke wangu mpendwa ambae kila mtu anamjua na tuko busy kujenga familia yetu inawezekana jambo haliwafurahishi baadhi ya watu hivyo kuamua kusambaza picha za zamani kwa nia zao ovu” aliandika Petitman
Hata hivyo Petitman aliendelea kusema kuwa huu sio muda wa watu kuchafuana bali ni muda wa kila mmoja kukaa na kujenga familia yake .
Imekuwa ni desturi kwa baadhi ya wasanii kuvujisha picha chafu bila kujulikana kwa chanzo cha picha izo zilipotokea ambapo kwa mwanadada Hamisa si mara ya kwanza sasa picha zake akiwa katika hali kama iyo kuonekana mitandaoni.