Kim Nana Afungukia Tetesi Za Bifu na Lynn
Video vixen maarufu kama Lilian Kessy ‘Kimnana’ amefunguka na kudai kuwa yeye na video queen mwenzake Irene Louis ‘Lynn’ hawana Bifu kama inavyodaiwa.
Tetesi za kuwepo kwa Bifu kati ya warembo hao zilizuka Baada ya warembo hao wawili wote kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kim Nana amefunguka kuwa watu wamekuwa wakizungumza mengi kuwa ana bifu na Lynn, lakini hawajawahi kuwa maadui hata siku moja na Lynn ni kama mdogo wake na hata wakikutana wanasalimiana vizuri na kuzungumza.
Lynn ni mshkaji wangu, hatuna bifu kabisa ndiyo maana hata hivi karibuni niliposti kipande cha video nikiwa naimba wimbo wake wa Chafu kwa lengo la kumsapoti hivyo wanaosema tuna bifu imekula kwao maana siyo kweli”.