Kesi Ya Wema Sepetu Yazidi Kupamba Moto
Upelelezi wa kesi ya kusambaza video za ngono mtandaoni inayomkabili Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu umekamilika na yupo tayari kwa ajili ya Kusomewa mashtaka ya awali.
Akiwa mahakamani hapo Mwanasheria wa Serikali, Glori Mwenda amesema,
Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na taarifa njema ni kwamba upelelezi wa shauri hili umekamilika, hivyo tunaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali, mshtakiwa huyu”.
Wema anatetewa na wakili, Ruben Simwanza, alifikishwa na katika kesi ya msingi anashtakiwa Oktoba 15, 2018 jijini Dar es Salaam.
Wema Sepetu anatuhumiwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wake wa kijamiii ambapo kupitia hatua hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali.