Kesi ya Wema Sepetu ya hairishwa baada ya upelelezi kukamilika
Jumanne hii Wema Sepetu na wakili wake waliweza kufika kotini kuskiza kesi ya malkia huyu wa filamu miezi miwili baada ya kusemekana anatumia dawa za kulevya.
Wema Sepetu aliweza kufika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam, ambapo hakimu mkuu aliwajulisha kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekamilika na mrembo huyo sasa amebaki kusomewa mashtaka baada ya kupatikana na msokoto wa bangi nyumbani kwake.
Hata hivyo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema kesi hiyo itaskizwa June 1, ambapo Wema Sepetu ataweza kujibu mashtaka yake kwa mara ya kwanza.
Wakili wa mrembo huyu hata hivyo akona imani kuwa watashinda kesi hii.