Kesi Ya Mwana FA, AY Dhidi Ya Kampuni Ya Tigo Yaendelea Mahakamani

Kesi iliyofunguliwa na wasanii wawili Mwana FA na  Ay katika mahakama ya Ilala jijini Dar Es Salam  dhidi ya kampuni ya Tigo kuhusu fidia ya shillingi bilioni 2.1 ambazo kampuni iyo iliamriwa na mahakama kuwalipa wasanii hao imekubaliwa kusikilizwa tena katika mahakama hiyo.

Mnamo April mwaka huu mahakama hiyo iliamuru kampuni ya Tigo kuwalipa wasanii hao  fidia kwa kosa la kutumia nyimbo zao huku wakikiuka sheria za  hatimiliki na hatishiriki  kwa kutumia kazi zao katika miito ya simu  bila kuwa na makubaliano wala ridhaa ya wasanii hao.

download latest music    

Nyimbo hizo ambazo ni Usije mjini ya  Mwana FA na  Dakika moja ya Ay zilikuwa zikitumiwa na wateja wa kampuni iyo kwa kuzilipia huku wasanii hao wakiwa hawanufaiki na kitu chochote.Baaada ya hukumu iyo wasanii hao walikuja kufungua tena kesi mahakamani kwa ajili ya utekelezaji.

Hata hivyo Tigo nayo iliamua kufungua kesi mahakamani hapo kwa madai kuwa hukumu iyo ilipaswa kujumuisha pia   kampuni ya Cellulant Tanzania Limited na ina haki ya kujibu madai ya wadai hao.

Wakili wa kampuni ya Tigo Bw.Mbwambo anasema kuwa Tigo iliomba kampuni ya Cellulant iwapelekee nyimbo za wasanii hao na kufanya hivyo bila wao kujua kama kampuni iyo ilikuwa na makubalinao yoyote na wasnii hao.Ingawa katika kesi iyo kampuni iyo pia ilikuwa na haki ya kujibu lakini katika hukumu haikujumuishwa ivyo Tigo wanadai kuwa mahakama ilisahau kuwajumuisha kampuni iyo katika madai.

Hata hivyo kupitia wakili wao Albert Msando, wasanii hao waliiomba  mahakama  kutupiliwa mbali  madai hayo na kusema kuwa endapo kampuni ya Tigo inataka kampuni iyo kuongezwa basi wanapaswa kukata rufaa.

Akitoa maamuzi ya kesi iyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahamakani hapo ,Ritha Tarimo amesema kuwa hoja ya kampuni iyo hazipaswi kuwasilishwa kama pingamizi.Ameongezea na kusema kuwa itakapofika wakati wa kusikilizwa kwa hoja hizo zitasikilizwa ili kuona kama kampuni iyo iliachwa kwa bahati mbaya au la.Hata hivyo kesi iyo itasikilizwa tena tarehe 18 Oktoba.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.