Kesi ya Babu Tale Yahairishwa, Arudishwa Tena Rumande
Mkurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection Babu Tale mapema leo alifikishwa mahakamani kufatia kesi ya madai dhidi ya Sheikh Hamis Mbonde baada ya Babu Tale kutumia masomo ya Sheikh huyo katika maswala yake ya kibiashara bila kuwa na hati miliki kutoka kwa mwenyew.
Babu tale ambae alikamatwa tangu siku mbili zilizopita amekuwa akifikishwa mahakamani hapo lakini hakimu aliyetoa hati ya kukamatwa kwake hayupo hivyo kufanya kesi hiyo kuhairishwa.
Babu tal alipewa hukumu ya kulipa fidia ya shilingi milion 250 lakini hakufuatilia hukumu hiyo kwa muda tangu mwaka 2013 na ndipo hakimu alipotoa hati ya kukamamtwa kwakwe tangu february mwaka huu lakini mtuhumiwa amekuwa akikosekana kila anapotumia hati ya kufika mahakamani au kukamatwa.