Kesi ya Agnes Masogange Kusogezwa Mbele Tena
Kesi ya mwanamitindo na video vixen wa muda mrefu , Agness Masogange imesogezwa mbele tena baada ya wakili wake kuomba kuhairishwa kwa kesi kwa sababu mwanadada huyo ni mgonjwa na amelazwa katika hospitali moja jijini Dar.
Agnes ambae amekuwa akifatilia kesi yake kwa muda mrefu sasa baada ya kuingizwa katika list ya watu maarufu nchini ambao walisadikika kutumia madawa ya kulevya.Kesi hiyo ambayo i ekuwa ikisikilizwa na kupangiwa tarehe mpya kila siku.
Hata hivyo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena mwezi ujao (april 4) na kuangalia ili kujua hatma yake.