Kejeli Za Hamisa Zinavyozidi Kumnufaisha Zari, Ni Baada ya Kumwita Changudoa
Bado mambo yamekuwa si mazuri kwa maadui wawili yaani Hamisa Mobeto na Zari kutokana na wivu walionao baada ya kila mmoja kutaka kuvutia penzi la msanii mkubwa Diamond Platinumz upande wake ingawa inaonekana kuwa mwanaume mwenyewe yuko sana upande wa Zari.
Kumekuwa na kelele nyingi na matusi baina ya watu hawa wawili tena kufikia hatua ya kuingia hadi watu wa karibu katika familia zao,hivi karibuni hamisa alipost katika mtandao wake wa snapchat na kumwita zari changudoa mzee jambo ambalo pia liliibua maneno mengi kwa mashabiki wa pande zote mbili.
Sio hali ya kawaida kwa mtu kuitwa hivyo na bado akaweza kukubali jambo hilo , lakini hii imekuwa tofauti kwa Zari kwa sababu hata baada ya kuitwa hivyo alijibu na kukubali kuwa ni kweli yeyey ni changudoa mzee lakini uchangudoa alionao ndio umemfanya yeye kuwa pale alipo kama Bossy lakini uchangudoa wake ndio uliomfanya aweze kukaa na mwanaume ambae wanamgombania.
Katika ukurasa wake huu wa snapchat, Zari The Bossy alijibu tuhuma za kuitwa changudoa kwa kusema Bora mimi changudoa mzee mwenye mafanikio na bado ananipenda sana kuliko wewe kijana mwenye miaka 20, mama uliyeacha mara mbili na tuzo juu.
Zari amekuwa akionyesha mali zake na mijengo yake aliyonayo katika nchi mbalimbali ikiwepo afrika ya kusini,na amekuwa akijinadi kuwa pamoja na kwamba mke mwenzake huyo amekuwa akimwita changudoa ni wazi kuwa yeye ni changudoa na amekuwa na mafanikio kwa sababu hiyo.
Katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakipokea maneno hayo kwa taswira tofauti na hata wengine kuwa wanamshauri sana Hamisa kuacha kugombana na Zari kwa sababu amekuwa akimzidi sana katika nyanja zote tena hasa swala zima la mali na utajiri.
Hii ni faida kwa zari kwa sabau kila anapovamiva kwa matusi na Hamisa amekuwa aikubali na kufanya kupata sapoti kubwa ya mahabiki kuwa yeye hataki kumlipiza vibaya Hamisa bali kukubali kila anachoambiwa.