Keisha:Kurudi Kwangu Hakuhusiani Na Kiki Za Dogo Janja
Mwanadada wa muziki wa bongo fleva Khadija Shabani maarufu kama Keisha ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu kidogo amethibitisha kurudi tena katika muziki kwa kishindo kikubwa lakini sio kupitia kiki ya ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya iliyofanyika tarehe 28 Oktoba,
Akiongea na full shangwe ya Global ,mwanadada huyo anasema kuwa pamoja na kwamba siku ya harusi hiyo yeye pia alituma picha ya ndoa hiyo na kutangaza ujio wake mpyaahaimaanishi kuwa basi ndoa hiyo ni moja ya kiki zake za yeye kurudi katika game.
Ni kweli narudi kwenye muziki lakini ujio wangu hauna uhusiano wowote na kusambaa kwa picha ya Dogo janja na Irene Uwoya.
Keisha ambae siku ya harusi pia alikuwepo katika harusi iyo , aliweka post katika ukurasa wake wa instagram na kuwapongeza wawili hao na kusema kuwa watu pia wategemee ujio wake mpya kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuamini kuwa harusi ya wasanii hao ni kiki ya wimbo mpya wa mwanadada huyo.
Hata hivy siku ya Dogo Janja alipoamua kuongea kwenye media kuhusu ndoa yake hiyo aliambatana na Keisha ambae akithibitisha kuwa kuwepo kwa Kesiha katika ndoa hiyo ilikuwa ni kama mama mkwe wa bi harusi kwa sababu yeye na Dogo Janja ni kama mtu na mama yake ukizingatia kuwa yeye na Madee ni marafiki sana na dogo janja na madee ni kama mtu na mwanae.
hata hivyo Keisha amesema kuwa mashabiki wake wategemee kuja kwake na wimbo wake mpya lakini wasitilie maanani ile picha na ya harusi maana haina uhusiano wowote na nyimbo yake anayotaka kuitoa na hakuna hata kipande kimoja kitakachoonyesha harusi hiyo.
Hata hivyo wiki iliyopita alipoikuwa akiongea kwenye Clouds Media alisema kuwa yeye kuweka picha ile katika ukurasa wake ni kwa sababu picha ile iliwakutanisha watu wengi wa familia ya Tip-Hop ambayo ndio manejementi yake.