Kassim Mganga-Tusionee Wivu Mafanikio Ya Diamond
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kassim Mganga ameibuka na kumkingia kifua staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kuwataka watu wasimuonee wivu.
Diamond Platnumz anatajwa kuwa moja kati ya wasanii walioiweka Bongo fleva katika ramani ya kimataifa baada ya kufanya kolabo na Staa kutoka Naigeria Davido miaka Michache iliyopita.’
Mmoja kati ya wasanii ambaye amejitokeza na kumkingia kifua Diamond ni Kassim Mganga ambaye ameibuka na kuwataka Wasanii Wenzake na mashabiki kutomuonea wivu Diamond.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Kassim Mganga amefunguka haya kuhusu kipaji cha Diamond:
Tusimuonee wivu kwa sababu amefanikiwa sana, ila Diamond amebadilisha sana muziki wetu”.
Pamoja na kwamba Diamond sio mmoja ya wasanii ambao waanzilishi wa muziki wa Bongo fleva lakini anatajwa kuwa msanii ambaye amekuza na anaendelea kuikuza Bongo fleva.