Kala: Watanzania Wamemchukulia Dr. Shika Kama Kituko
Msanii wa Bongo fleva anayefanya mziki wake kwa miondoko ya hip hop, Kala Jeremiah amedai kuwa Watanzania wengi wanamchukulia Dr. Shika kama kituko Fulani.
Dr. Shika aliyepata umaarufu wiki chache zilizopita baada ya kununua nyumba za mnada za Lugumi kisha kushindwa kuzilipia amezidi kupata umaarufu huku watu wakiwa na maoni mbali mbali juu ya nini hasa ilikuwa nia ya Dr. Shika.
Mapema wiki hii mwanamuziki Kala aliibuka na kuwaomba watu wasimdharau Dr. Shika, lakini pia kwenye mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo, Kala amedai kuwa mpaka hivi sasa bado kuna Watanzania ambao bado wanamuona Dr. Shika kama kituko:
Mara ya kwanza nilipoona habari yake kusema kweli sikuielewa lakini baadae nilijaribu kuifatilia na mahojiano yalivyozidi kuendelea nikaona huyu jamaa hayupo kama watu wengi wanavyomchukulia kiwepesi lakini ukiangalia yule jamaa kapitia mambo magumu sana kwa hiyo lenfo language la kupaza sauti ni kuomba Watanzania wamuonee huruma kwanza na wampende kwasababu niliona kama wanamchukulia kama kituko lakini huwezi kuja yaliyomsibu mpaka kufika pale ni yapi kwa kusikiliza mahojiano yake na anvyoeleza kuwa alitekwa inaonekana sio uongo na kwa jinsi alivyotekwa na mate so aliyopata anaonekana kabisa kuwa kisaikolojia imemuathiri kwaiyo kwa kujua hilo watu lazima wampende wamuweke karibu kama mtu aliyepata matatizo kwaiyo asipuuzwe kwasababu ni mtu anayeonekana anaweza akawa na mchango mkubwa kwa taifa letu”.