Kajala Atangaza Kujiweka Mbali na Mabifu Kwa Mwaka Mpya
Staa wa filamu za Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa amedhamiria kuumaliza mwaka 2018 vizuri bila mabifu na watu na pia kuuanza mwaka 2018 vizuri.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Kajala amefunguka na kusema kuwa anamuomba mno Mungu aanze mwaka ujao akiwa hana adui na hata kama kutakuwa na mtu amemkosea, ataenda kumuomba msamaha kwa sababu anataka kufunguliwa mambo yake.
Kabla ya kumaliza mwaka huu, sitaki kuwa na bifu na mtu na hata kama kuna mtu nitakuwa nimemkosea, nitamfuata mwenyewe na kutaka mwaka unaokuja tuuanze vizuri, mambo ya mabifu yanafunga bahati na mambo mazuri“.
Kajala ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa na mwaka mzuri wa 2018 ikiwemo kuwa na kazi nzuri na kujiheshimu kwa kuepuka skendo kwenye mitandao ya kijamii.