Kajala Akanusha Kutumika Vibaya Na Wasanii
Kajala Masanja msanii wa Bongo Movie pia ni balozi wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko unaoendelea sasahivi kote nchi ambae hivi karibuni amekuwa akituhumiwa na tetesi nyingi ikiwepo wa kutoka na wapenzi wa wasanii wenzie , huku wengine wakimwita “nyakunyaku” , amefunguka tena na kuongelea swala ya yeye kutuhumiwa kutembea na wasanii wa Bongo fleva ambao wanamtumia vibaya kwa ajili ya kutafuta kiki ya kutaka kujulikana na kupata majina katika kazi zao kupitia yeye.
Katika mahojiano yake na Channel ya EATV katika kipindi cha eNews,alisema kuwa sio kwamba anatumika na wasanii bali kuna baadhi ya wasanii ni watu wake wa karibu.
Kajala alipoulizwa kuhusu msanii Peter mc ambae aliimba wimbo na kutaja jina la Kajala na kusema baadhi ya maneno yanaonyesha kama wapo kwenye mahusiano. Hata hivyo Kajala alipoulizwa kuhusu msanii huyo alishangazwa kuwepo kwa nyimbo iyo bila yeye kuijua au hata watu wake wa karibu kumwambia kuhusu msanii huyo na wimbo wake, kwa kifupi anasema hamjui msanii wala wimbo.Kwa kuongezea Kajala alisema kuwa endapo atausikia wimbo huo atafatilia na kuongelea swala ilo.
Hata hivyo kulikuwa na tetesi za Kajala kutembea na msanii mwingine wa Bongo Fleva , Country Boy ambapo kwa kipindi cha nyuma msanii huyo wa Bongo Fleva alipoulizwa kuhusu habari hizo alisema kuwa yeye na kajala ni kama mama na mtoto, kwa kulifafanua swala ilo Kajala amesema kuwa watu wanakuwa wanaongea vitu bila kujua , yeye na Counrty Boy ni kaka mama na mtoto kwa sababu alishawahi kumsaidia katika maswala yake ya muziki na uhusiano wao umebaki kuwa hivyo “Country mimi ni mtoto wangu, na huwa haniiti Kajala, ananiita mama , kitu watu hawajui ni kwamba wimbo wa kwanza kabisa wa Counrty mimi ndio nilimpeleka kwa Lamar nikamlipia na akafanya‘ ameongea Kajala
Kajala anaonekana kukerwa na tabia za watu kuzusha mambo , kila unaetembea nae barabarani basi ni mtu wako” watu tutashindwa kutembea na ndugu zetu , watu wanakwambia unatoka nae, basi utatembea na kila mtu humu duniani” anaongezea kajala