Kajala Akana Tetesi za Kurudiana na Pfunk Majani
Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amekataa kata kata tuhuma za yeye kurudiana na Baba mtoto wake Producer mkongwe wa muziki nchini, P Funk Majani.
P funk na Kajala walikuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka ya nyuma mpaka wakajaaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Paula lakini waliachana muda mrefu uliopita.
Siku za hivi karibuni Kumekuwa na tetesi kuwa Kajala na P funk wamerudisha penzi lao la siku nyingi na kuamua kuitunza familia pamoja huku fununu hizi zilizmshwa baada ya Kajala kutupia video kwenye mtandao wa SnapChat akiwa na P funk.
Baada ya tetesi hizo kuanza kusambaa Kajala aliongea na Global Publishers na kuweka wazi kuwa hajatudiana na P funk wala hawezi kurudiana naye:
Jamani siwezi kurudiana na P, yule atabaki tu kuwa mzazi mwenzangu. Hiyo video tulikuwa tumeenda shule kwenda kumuona mwanetu Paula baada ya hapo kila mtu alichukua hamsini zake”.
P funk amekuwa kwenye uhusiano na mwanamke mwingine kwa miaka mingi ambaye amezaa naye mtoto mmoja.