Kajala Adaiwa Kuvunja Ndoa Ya P Funk
Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amekumbwa na skendo nzito baada ya taarifa kusambaa kuwa amerudiana na Baba mtoto wake ambaye ni prodyuza mkongwe wa muziki nchini P funk.
Kwa kipindi hiki kifupi Kumekuwa na tetesi zinazotembea na kudai kuwa Kajala na P funk wamerudiana ingawa Kajala alikataa tuhuma hizo lakini mke wa P Funk alimtolea povu Instagram na kudai katelekezwa na P funk ambaye amerudisha majeshi kwa Kajala.
Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa mtoa habari wao wa Kuaminika amewapa taarifa kuwa ndoa ya P funk imetifuka vibaya mno na inadaiwa mkewe Samira amecharuka baada ya kupata taarifa mumewe amekuwa akionekana na Kajala.
Ndoa ya P-Funk kwa sasa inawaka moto kwa kweli maana hakuna maelewano kabisa na mkewe ana mimba kubwa tu ya mtoto wa tatu na vurugu zote hizo zimesababishwa na Kajala ambaye anasemekana amerudiana na mzazi mwenzake huyo ambaye kabla ya kuachana walijaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kike ambaye ni Paula,” alivujisha mchapo mtoa taarifa.
Baada ya tuhuma hizo gazeti hilo lilimsaka Kajala ambaye alifunguka haya:
Nashangaa kwa nini huyo mke wa P-Funk hajiamini wakati anatarajia kuzaa mtoto wa tatu sasa, mimi sijarudiana naye ila huyo ni mzazi mwenzangu tu, namsihi ajiamini maana huyo ni mume wake tu.”
Tetesi hizo zilizopita kusambaa baada ya Kajala kutupia picha ya P funk na mtoto wao PAula wakiwa wanaogelea ambapo alimtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa.