Juma Jux Atinga Ndani Ya Coke Studio
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux amefanikiwa kufika katika bonge la shoo la Coke Studio ambalo limeshawahi kuwashirikisha wasanii wakubwa Afrika.
Jux anafanya vizuri na ngoma zake kama vile Zaidii” na “Tell Me”, Lakini mbali ya muziki, Jux pia ni mfanyabiashara akiwa ni mmiliki wa chapa ya T-shirts “AFRICAN BOY”, ni bidhaa za nguo zinazopatikana Afrika Mashariki zikimilikiwa na mwimbaji pamoja na mtunzi Juma Jux.
Jux amesema kuwa moja ya mipango yake kwa mwaka 2019 ni kufanya nyimbo nyingi za kushirikiana na wasanii kutoka nje ya Tanzania. Katika Coke Studio Jux anashirikiana na mwana dada Shellsy Baronet kutoka Mozambique.
Kwenye interview yake aliyofanya Jux amefunguka Mengi juu ya mara yake ya kwanza Kushiriki kwenye msimu mpya wa Coke Studio:
Coke Studio ni jukwaa zuri kwa wasanii kwani inapelekea kubadilishana tamaduni na nchi zingine; ni kitu kizuri ambacho nafurahi kuwa sehemu ya Coke Studio.”
JUMA JUX ataiwakilisha vyema chapa ya “AFRICAN BOY” katika jumba la Coke Studio kwa mwaka 2019, kuanzia Februari.