Jokate:Napenda Watu Wanijue Kutokana Na Kazi Ninazofanya
Mwanadada mrembo ambae amekuwa akifanya kazi nzuri katika jamii hasa ya kurudisha fadhila na kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii amefunguka na kuongelea vitu ambavyo vimekuwa vikimkera hasa katika matumizi ya mitandao na maswali ambayo amekuwa akiulizwa na waandishi wa habari kuhusu maisha yake.
Jokate amesema kuwa ukiachana na yeye kuwa maarufu lakini hapendi kwenda katika interviews na kuanza kuulizwa maswali binafsi yanayohusu maisha yake ya ndani na ndio maana amekuwa ni mtu asiependa kuwaweka ndugu na watu wake wa karibu katika mitandao ya kijamii labda iwe ni kikazi au swala linalomlazimu kufanya hivyo.
Hata hivyo Jokate amesema kuwa anapenda watu wamjue na kumuongelea zaidi kuhusu mambo anayoyafanya katika jamii yeye na brand yake na sio maisha yake binafsi.
Sipendi kuulizwa kuhusiana na maisha yangu binafsi na hata ukiangalia katika page zangu siposti mchumba, siposti wazazi na wala siposti nduguy kivile kwa sababu najua ukishawapost unakuwa unawaweka katika situation ya watu kutaka kuwaongelea na kama unavyojua watu wengi online wanakuwa na uwezo wa kuongelea kitu chochote kile kwaio napenda kuwalinda sana watu wangu wa karibu, lakini pia napenda watu wanijue kupitia kazi zangu na vitu vya muhimu ambavyo nimekuwa nikivifanya kwa jamii yangu na vitu kama hivyo – Aliongea Jokate alipokuwa akiojiwa na Millard Ayo Tv
Jokate ambae hivi karibuni amekuwa akionekana akifanya mabo mengi yanayohusiana na jamii amesema kuwa anataka kuwa mfano wa kuogwa kwa mambo mengine mazuri na ndio maana hataki kuwa anaweka maswala yake binafsi katika media.
Hata hivyo ni wachache tena hasa watu maarufu kama Jokate wanaoweza kuendesha maisha yake hasa binafsi kwa siri kubwa, tangu Jokate isemekane kuwa ameachana na Ali Kiba amekuwa kimya sana kutaka kuwaonyesha watu mahusiano yake ya kimapenzi hadharani.
Jokate anapaswa kuwa mfano wa kuigwa sio kwa watu maarufu tu lakini pia kwa watu wote ambao waliweza kupewa nafasi ya kujulikana na bado wakaichezea nafasi hiyo, ukiachana na urembo ambao Jokate umekuwa ukimfaidisha lakini sasa Jokate ameamua kurudi na kusaidia jamii yake katika maswala mbalimbali yanayoikabili ikiwepo na sekta ya elimu.