Jokate Atumbuliwa Uongozi UVCCM
Mwanadada mrembo na mjasiriamli Tanzania, Jokate Mwegelo ametenguliwa uongozi katika chama cha mapinduzi, nafasi alikuwa ameteuliwa mwaka jana kuwa katibu Mwenezi wa uhamasishaji kwa vijana uvccm.
Utenguzi huo ulifanyika March 25 katika kikako cha dharura kilichofanyika jijini baada ya kamati kuu ya uvccm ikiongizwa na Denis James ambae ni mwenyekiti wake kuamua kumtoa uongozi huo dada huyo.
Hata hivyo mpaka sasa bado haijafahamikani kwa nini mwana dada huyo ametenguliwa cheo hicho, lakini kwa katiba na sheria zao viongozi husika wanayo mamlaka ya kufnya hivyo.
Ikumbukwe kuwa baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo, Jokate aliweza kufanya shughuli nyingi zaidi za kijamii kupitia chama chake na alihaidi kufanya mengi zaidi.