Jokate Aonyesha Mahaba Yake Kwenye Soka
Sio tu kwa sababu ni mwanamitindo basi ajikite huko, kumbe ukiachana na siasa na ujasiriamali bali pia mwanadada Jokate Mwegelo anapenda sana mpira na kwa kutibitisha ilo ameonyesha timu anayoipenda na pia mchezaji wa mpira anaemkubali katika soka.
Katika baadhi ya post zake Jokate alishawahi kusema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa taem ya arsenal lakini hakuwahi kusema wazi ni mwanasoka gani amekuwa akimkubali kati yao.Katika ukurasa wake wa instagram, Jokate ameandika kuwa anamkubali sana Ronaldo na kusema kuwa mwanasoka huyo anakipaji kikubwa kuliko Messi.