Johari Kuingia Rasmi Kwenye Siasa 2020
Msanii wa bongo movies Johari Chagula amefunguka na kuonyesha nia yake ya dhati ya kutaka kuingia katika siasa hasa mwaka 2020 huku akisma kuwa lazima atagombea nafasi ya ubunge.johari atokuwa msanii wa kwanza kujiingiza katika siasa lakini inakuwa inategemea ni kwa kiasi gani anakuwa anataka kusaidia jamii yake.Akiongea katika kipindi cha kikaangoni Live cha Eatv, Johari alisema kuwa kamwe hawezi kuiacha ccma na kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa ccm ni lazima aagombea ubunge mwaka 2020.
nina mapenzi makubwa sana na chama changu cha CCM, na nina mpango mwaka 2020 nitagombe a ubunge na nia ninayo n apia uwezo ninao.sihitaji kiviongelea hivi vitu sana kwa sasa ila muda wa kuvifanya ukifika tu nitakuja kuviongelea.
Johari anasema kuwa hataki kuchanganya sana kazi zake za sanaa na mambo ya siasa kwa sababu mashabiki wake ni wa vyama tofauti na hataki kuwagwa hata kidogo.hivyo anaomba kuwa anapokuwa katika siasa atambulike kama blandina na akiwa katika sanaa basi ajulikane kama Johari , jina ambalo limempa umaarufu katika sanaa.
Wasani wengi we waliowahi kuingia katika siasa ni pamoja na Irene Uwoya, Wema Sepetu ambao waligombea katika majimbo yao lakini kura za maoni hazikutosha hivyo walibaki kuwa wanachama wa kawaida .lakini pia kuna mwanadada Jokate ambae kupitia siasa ameweza kusaidia jamii yake kwa kutumia nfasi kubwa aliyonayo.