Johari Aipa Baraka Zote Ndoa Ya Ray na Chuchu Hansy
Muigizaji wa Bongo movie Johari Chagula ametoa baraka zake zote kwenye ndoa ya Ex wake Ray Vincent Kigosi na mama mtoto wake Chuchu Hansy.
Johari na Ray walikuwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi kipindi cha nyuma lakini ameibuka na kuweka wazi kwa hivi sasa hana kinyongo na wapendanao hao kuwa pamoja.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Johari amedai kuwa hakuna kitu kitakachomfurahisha kama mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ akimuoa mzazi mwenziye, Chuchu Hansy.
Lakini pia Johari ameweka wazi kuwa Chuchu ni chaguo sahihi la Ray maana ni mwanamke ambaye amemzalia mtoto mzuri.
Kiukweli nitafurahi sana mkurugenzi mwenzangu (RJ Company) akimuoa Chuchu. Kwanza ni mwanamke wa chaguo lake na pia amemzalia kidume cha nguvu na kwenye harusi nitakuwa mstari wa mbele“.
Ray na Chuchu Hansy wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden.