Jinsi Waaandishi wa Habari Walivyomtolea Povu Diamond Platinumz.
Hivi karibuni msanii diamond platinumz amefungua rasmi kituo chake cha habari ambacho kitakuwa na radio na tv, lakini waandishi wa habari kutoka tanzaia wamemjia juu msanii huyo kwa kitendo chake cha kwenda kutafuta waandishi wa habari na wafanyakazi wa radio hiyo mtaani bila kujali kuwa kuna vigezo na masharti ya habari.
Waandishi hao wanasema kuwa kazi ya uandishi wa habari inatakiwa kuwa na proffesional yake kwaio alichokifanya Diamond sio kitu sawa kabisa na hajafanya vizuri.
Akiongea na online tv, mmoja wa waandishi wa habari wa gazeti penda hapa nchini Chritopher Lisa ambae ni mwandishi wa habari anasema kuwa
swala la dimaond kwenda kuatafuta wafanyakazi mitaani kwa ajili ya radio na tv yake mi naona ni kama vile amekos watu wa kumshauri kwa sababu uandishi wa habari ni taaluma kama zingine,taaluma hiyo inahitaji watu waliosoma na ambao wamekidhi vigezo vya habari kwa mfano sasa hivi tuna sheria kuwa watu wa habari ni lazima wawe hata na diploma tu,ambapo serikali ilitoa miaka mitano kwa waandishi kwenda kusoma.
kitendo cha diamond kwenda kutafuta waandishi nje ya taaluma ya habari sidhani kama kitamsaidia sana kwa sababu kutangaza sio kwamba ni sanaa au muziki ule kusema kuwa utatumia kipaji chao. kuna taratibu , sheria na kanuni za kuzungumza na hata kuongea pia sio unaongea tu blaah blaah…
Mwandishi mwingine ambae pia aliguswa na jambo hilo alisema;
Kutafuta watangazji kwa kutumia njia ya viapaji ni kosa kubwa sana kwa sababu kwa jinsi a ambavyo sasa hivi tanzania tunaelekea katika mfumo wa kuatambua taaluma ya mwandishi wa habari sasa unapochukua watu bila taaluma madhara yake ndo haya sasa unashangaa kwanini kuna habari fulani imetokea ni kwa sababu watu hawana taaluma na hawajafata mchakato wa upatikanaji habari.Namshauri diamond afany matangazo ya kazi na watu wafanye interviews.
Moja ya mwanafunzi na shabiki wa diamond alisema
kwa mfano kama mimi ninavyosomea IT, Nikisema kuwa nataka kufungua mgahawa wa kuhusu maswala ya kumputa basi ni lazima nitaajiri watu waliosomea kitu ninachotaka kukifanya.