Jacqueline Wolper atokwa na machozi baada ya kuona jinsi vijana walivyong’ang’ania nafasi za kazi
Ukosefu wa ajira nchini ulidhihirika hivi karibuni wakati TRA ilitangaza nafasi za kazi. Maelfu ya vijana walijitokeza kuwania nafasi chache za kazi ambazo zilitangazwa na TRA.
Jacqueline Wolper aliweka picha ya vijana waliojitokeza jana katika usaili wa kazi TRA na kuandika ujumbe mrefu akieleza namna alivyoguswa;
“Nikiangalia picha kama hizi naumiaga sana nanilivyo na machozi ya karibu basi nalia kabisa…?
Yaani naona hata wadogo zangu miongoni mwa hawa wanaopigania nafasi yakupewa kazi
Na ukizingatia nimesomesha wadogo zangu kwa tabu sana tena nilikuwa sina hata biashara huku nikisaidiana na wazazi wangu.
Roho inakuuma pale ambapo mdogo wako anakwambia Dada nimepata kazi ya kujishikiza kwa weeki tatu nitalipwa laki na nusu kule Mbeya kijijini tena hapo ni uliyefikiria akipata degree yake atakuja japo kutuinua ama lah! Basi ajitegemee mwenyewe Dah!
Yaani najiskiaga hasira siku moja mpaka nikamsema mdogo wangu..bila kujua kumbe anaumia anatamani muda na pesa tulizopoteza hata apate wakati wakulipa fadhila na sisi tucheke natujue umuhimu wake kwetu lakini ndo hivyo… Maskini ukimwambia subiri utapata kazi hakuelewi anakuona unampotezea muda..anaishia kukujibu basi Dada we unajulikana niombee kazi ?
Mimi najiuziliza unaposema ipo siku ipo siku sijui hiyo siku ni ipi… haya hapa wote hawa wanaohitajika ni wachache (yaani kwa uwiano ni kama mtu mmoja achaguliwe kati ya watu 140) kwasababu ni watu 56,000 kwa nafasi 400…(kama data ziko sahihi) …ohh my God…
Bora hata huyu mdogo wa Wolper ataomba kaela kavocha nakula na kulala atapata vipi waliosomeshwa na wazazi wakambo au kwa msaada??? au ambao wanapotokea hakuna hata lingine??. Aisee polen sana ndugu zangu na nyinyi mliopata kazi basi heshimuni saana sana kazi zenu. Nawaombea na mabosi pia wawafikirie.”