Isabela Mpanda: Nilikuwa Nalala na Godzilla
Msanii wa Bongo movie na Bongo fleva Isabela Mpanda maarufu kama Bella Fasta ameibuka na kuweka wazi alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Marehemu Godzilla.
Isabela ambaye ameonyesha kuguswa na msiba wa rafiki yake huyo wa karibu, amekuwa akiposti picha mbalimbali kwenye ukurasa wake wa Instagram ambazo alikuwa pamoja na Zilla na kudai moja ya shati alilokuwa akivaa Zilla hata yeye Isabela amekuwa akilivaa huku akitupia picha.
Lakini pia Isabella ameweka wazi kuwa kwenye moja ya picha zake kuwa yeye Ndiye alikuwa Mpenzi Wake na hata kudai walikuwa wanalala wote na kuamka wote.
Lakini stori ya Isabela imeibua maswali mengi kutoka kwa watu kutokana na kutofautiana ya familia ambapo yeye alisema kuwa Mpaka Marehemu anafikwa na mauti hospitalini Lugalo alikuwa anawasiliana naye mpaka dakika za mwisho Lakini Familia yake imedai kuwa Godzilla alifariki nyumbani kabla hata hajafika hospitali.