Irene Paul- Siwezi Kumlazimisha Mtoto Wangu Kuwa Msanii
Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul ameibuka na kuweka wazi kuwa ingawa yeye ni Msanii na anaipenfa kazi yake Lakini hawezi kumlazimisha Mtoto Wake awe hivyo pia.
Irene Paul amefunguka hayo alipokuwa anamuongelea Mtoto Wake mdogo Wake kike anayeitwa Wendo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Irene aliongelea mipango ya mwanaye na kama endapo atafuata nyayo za mama yake na yeye kuwa msanii.
Unajua mwisho wa siku staa ni mimi, yeye si staa hivyo napenda aishi maisha yake mwenyewe anayoyapenda, ajifunze vitu tofautitofauti, akifika umri mkubwa atachagua la kufanya mwenyewe na staili ya maisha yake mwenyewe kwani wakati huo huenda na mimi nitakuwa si staa tena”.
Hivi sasa Irene Paul anang’ aa kwenye tamthiliya ya Huba ambayo inarushwa na kituo cha DSTv ambapo amecheza Sambamba na wasanii wengine.