Inspector Haruni Ajipanga Kurudi Upya Kwenye Muziki.
Msanii mkongwe Inspector Haruni ameongelea swala la yeye kupotea katika game kwa muda mrefu ikiwa wenzake kama Professah Jay, Lady Jay Dee na hata Juma Nature bado wapo kweye game na wanafanya vizuri.
Inspector Haruni anasema kuwa sio kweli kuwa wasanii wakongwe wamefunikwa kikazi na wasanii machipukizi ila tu mfumo wa maisha unaenda unabadilika sana kwaio wanajipanga na kurudi tena hivyo wakae mkao wa kula.Msanii huyo anasema kuwa wasanii wengi wa zamani wapo kimya kwa sababu wanajipanga ili kurudi tena kwa sababu wasanii wengine wa sasa wameshaweza ku-copy na maisha ya sasa tofauti na wao waliokaa kimya muda mrefu hivyo inabidi wajipange.
unajua kuwa muziki umebadilika sana,siyo sawana tulivyokuwa tunafanya zamanikwanza gharama za studio tu kwa sasa ni kubwa lazima mtu ujipange , pia kwenye nyimbo lazima tuwaze sana ili tujue tunaimba nini kwa sababu unakuta muziki unakufa kwa sababu
nilikuwa kimya kwa sababu mimi nilikuwa najipanga nasasa narudi tena kwenye gamehakuna mwanamuziki yoyote wa sasa anaeweza kutushinda sisi wakongwe maana muziki wao ni mwepesi na haudumu kwa muda mrefu kama zamaani lakini ukiangalia nyimbo zetu za zamani zikipigwa sasa hivi utaona bado zinawika na zinatoa ujumbe wa maana.
Inspector Haruni ni moja wa wasanii wakongwe waliokuza muziki miaka ya 90,hata hivyo mapinduzi makubwa ya muziki wa bongo fleva yaliyofanyika katika muziki huo yaliwafanya wasanii wengi kuwa kimya lakini bado wanaamini kuwa style yao ya muziki ni imara zaidi hivyo hata wakirudi wtapokelewa vizuri na mashabiki.