Idris Sultan Alamba Shavu Nono
Muigizaji wa Bongo movie na komedian maarufu Idris Sultan amedaiwa kulamba shavu nono katika ulimwengu wa Burudani Baada ya safari yake ya nchini Afrika ya kusini.
Global Publishers wanaripoti kuwa Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la Komedi lililoandaliwa na Comedy Central, moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini.
Mwaliko wa Idris unakuja baada ya mafanikio makubwa katika Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu ya wapenzi wa comedy hapa nchini.
Kwenye mahojiano aliyofanya na GPL, Idris alisema lilikuwa na lengo kuu la kuburudisha na kuelimisha watu katika maswala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.
Tarehe 1 Desemba, Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki jijini Dar ambapo watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket.
Sex Tour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa ya muziki”.