Idris Sultan Afungukia Tetesi Za Kujisogeza Kwa Mobetto
Staa wa filamu aina ya Komedi, Idris Sultan amefungukia tetesi zinazomkabili za kujisogeza kwa mwanadada anayetrend Hivi sasa kwenye Mitandao ya kijamii Hamisa Mobetto.
Tetesi hizo zilianza kusambaa Baada ya Idris kuonekana akikomenti sana kwenye picha za mrembo huyo mara tu Hamisa anapoposti picha zake basi Idris anekuwa akimuachia makopa tu.
Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa, Idris kwa sasa ameamua kujipooza kwa Mobeto.
Wamekuwa wakiongozana kila kona kama kumbikumbi, ndiyo kwanza mapenzi yao yanachipukia“.
Baada ya tetesi hizo kusambaa, Gazeti hilo lilimsaka Idris ili kuupata Ukweli wa mambo kutoka kwake ambapo moja kwa moja alikana kabisa tetesi hizo na kumwaga povu:
Hebu acheni mambo yenu ya ajabu bwana kwa hiyo kila msichana nitakayeongozana naye basi ni mpenzi wangu? Halafu mmesahau kwamba mimi na Hamisa ni washkaji kitambo tu? Sasa kwa nini leo muanze kusema natoka naye? Muda mwingine watu wakikosa kazi ya kufanya huwa wanatunga tu vitu vyao”.