Idris Aifurahia Sex Tour, ni Zaidi ya Comedy
Mchekeshaji maarufu anaezidi kupanda kwa kasi katika tasnia ya sanaa upande wa vichekesho vya jukwaani ,Idris Sultan amefunguka na kusema kuwa wazo lake la sex tour limezaa matunda makubwa kuliko hata vile aliwaza hapo awali.
Idris anasema kuwa sex tour imekuwa tamsha kubwa kuwahi kutokea nchini lenye mafanikio zaidi hata matamasha ya muziki nchini na ndio sababu iliyomfanya kupata hata dili kubwa huko Afrika ya kusini.
Idris amepata mualiko na dili kubwa afrika ya kusini katika central comedy ya nchi hiyo huku akisema kuwa baada ya kuona amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sex tour ambapo alianza kwa kuhamasisha vijana kujua afya zao na kisha kuanda kipindi cha comedy kwa mashabiki zake lakini cha kushangaza ni kwamba walijitokeza watu wengi hata wengine kukosa ticket.