Huyu Hapa Mwakilishi Wa Miss World Kutoka Tanzania
Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu waziri wa habari na michezo Dr.Alison Mwakyembe kuongelea jinsi uhujumi unavyofanyika katika mashindnao ya Miss Tanzania nchini na kusema kuwa kumekuwa na uongo mwingi sana unaondelea katika kuuanda mshindano hayo, hata hivyo mashindano hayo ambayo mpaka sasa yalipaswa kuwa yamefanyika ili kumpuzisha aliyeshindwa mwaka jana na kama ilivyo desturi kuwa ni Miss mmoja kwa mawaka mmoja.
Mashindano ya Miss World yanakaribia kufanyika huku profiles za mashindano hayo zikiwa zimeshafunguliwa, Tanzania ikiwa kama moja ya washiriki tayari walishapata mshiriki atakae wakilisha katika mashindano hayo anaejulikana kama Julita kabete, Ingawa sasa kumekuwa na maswali je, Miss Tanzania haitafanyika tena, na je imekuwaje kupatikana kwa mshiriki wa Miss World bila kuandaa mashindano haya Tanzania.
akiongea na eNews ya Clouds Tv, Godfrey Mungereza, katibu mtendaji wa BASATA, amefafanua kwa kina jambo ilo na kuwaelewesha wanahoji kuhusu ilo na juu ya uhalalai wa Julita”tumetoa kibali cha muda kwa julita kabete,ivyo hatatuwakilisha katika mashindano”
Alipoulizwa kuhusu vigezo gani walitumia kumchagua Julita ilhali hakuna mashindano yoyote yaliyofanika mwaka huu kuchagua Miss Tanzania , Mungereza alisema kuwa “Vigezo huwa ni kutoka tano bora, na tunaangalia kama anaweza kutuwakilisha vyema katika mashindano hayo,na pia kikubwa tunachoangalia ni kama mrembo huyo bado anakuwa ana mustakabali wa kuendelela kushiriki mashindano“aliongezea katibu huyo.
Hata hivyo Godfrey Mungereza alisema kuwa sio kweli kuwa mashindano ya Miss Tanzania hayatafanyika tena ,bali lazima yale mapungufu kwanza yaweze kutatuliwa kabala halijawa tatizo.Akitolea mfano wa mashindano yaliyofanyika mwaka jana , ambapo Miss Tanzania alisaini hati ya gari kama zawadi lakini gari ilo lilikuwa ni hewa maana zawadi hiyo haikuwepo katika uhalisia.
Miss Julia Kabete, alikuwa ni mshindi wa Miss Ilala mwaka 2016 ambapo pia alipata bahati ya kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo na kuwepo katika washindi watano bora za ,Miss Tanzania ambapo katika mashindao hayo alishinda Diana Fleva.Juliata Kabete pia ndio Miss aliyekabithiwa bendera ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Africa mwaka 2016 yaliyofanyika kwa mara ya kwanza kabisa nchi Nigeria.
Julita Kabete alipokuwa anakabithiwa Bendera ya Tanzania mwaka 2016 na aliyekuwa Waziri wa Habari na Michezo Mh. Nape Nnauye , kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Africa yaliyofanyika nchini Nigeria
Muonekano wa Julita Kabete.